Jeremiah 2:10-13

10 aVuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu
Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania.
nawe uangalie,
tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,
uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.
11 cJe, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?
(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)
Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao
kwa sanamu zisizofaa kitu.
12Shangaeni katika hili, ee mbingu,
nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”
asema Bwana.
13 d“Watu wangu wametenda dhambi mbili:
Wameniacha mimi,
niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,
nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,
visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.
Copyright information for SwhNEN